MAGABA SECONDARY SCHOOL

 Namba ya usajili: S4524 Kituo cha mitihani: S 4810 P4809

 

 

S. L. P 264 Kasulu – Kigoma – Tanzania

Simu: 0767 322707/ 0756 555 011 / 0752 486 955,

Barua pepe: magabasecondary@gmail.com

 

Mahali shule ilipo ni Kasulu barabara ya Kibondo Jirani na Kijiji cha Nyakitonto.

 

MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2023.

Jina la mwanafunzi. ____________________________________________

Uongozi wa Shule ya Sekondari Magaba unapenda kukutaarifu kwamba umekubaliwa kujiunga na Kidato cha kwanza katika Shule hii kwa mwaka wa masomo 2023. Magaba Sekondari ni Shule ya bweni tu kwa wavulana na wasichana; Shule ipo Wilaya ya Kasulu, Mkoani Kigoma umbali wa kilometa ishirini toka Kasulu mjini barabara iendayo Mwanza (Kibondo Road).

 

Shule itafunguliwa tarehe 07 Januari 2023 siku ya Jumamosi hivyo unapaswa kuwahi mapema shuleni kabla ya saa kumi jioni.

 

Magaba Sekondari ni Shule iliyosajiliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa namba S4524, namba ya kituo cha Mtihani wa Taifa ni S4810 na namba ya kituo kwa wanafunzi wa kujitegemea (Private Candidates) ni S4809.

 

Shule inafundisha masomo yote ya msingi ambayo ni:-

Civics, History, Geography, Kiswahili, Englisha Language, Physics, Chemistry, Biology, Basic Mathematics na Literature in English.

Maabara zote za masomo ya sayansi zipo, tunao walimu wa masomo yote wenye uzoefu wa kutosha na wachapakazi. Maadili yanafundishwa kupitia elimu ya dini Shuleni kwa madhehebu yote. Uhuru wa kuabudu unapewa kipaumbele kwa siku husika na dhehebu husika na ibada za kila siku jioni zinazingatiwa na kusimamiwa ipasavyo.

Unatakiwa kusoma na kuelewa sharia na taratibu za shule. Pia utajaza fomu zote, F. 01, F. 02 na F.03 kama zinavyoelekeza na kuzileta shuleni siku ya kuripoti. Fomu hizi zimeambatanishwa na barua hii.

Unatakiwa kujaza fomu zote, F1, F2 na F3 na kuzileta shuleni siku ya kuripoti. Fomu hizi zimeambatanishwa na barua hii.

KARIBU SANA MAGABA SEKONDARI KWA ELIMU BORA.

 

Wako katika elimu

 

-------------------------

        Mkuu wa Shule

 

 

 

 

1. 0 ADA (KARO) NA MAHITAJI YA SHULE:

Ada ya Shule ni shilingi za Kitanzania 1, 300, 000/= (million moja na laki tatu tu)

 

       1. 1 ADA INALIPWA KWA AWAMU NNE KAMA IFUATAVYO:-


·        Januari                        500, 000/=

·        Aprili                           200,000/=

·        Julai                             400, 000/=

·        Septemba                   200, 000/=


 1.2 MICHANGO MINGINE

Huduma ya kwanza na uthibiti ubora wa shule pamoja na UMISETA ni Tsh.50, 000/=

Ada ya shule tu ndiyo ilipwe kwenye mojawapo ya akaunti za Shule, aidha kupitia

NMB A/C NO: 51410004076 au CRDB A/C NO: 0150227648600

Jina la akaunti zote ni MAGABA SECONDARY SCHOOL.

Mwanafunzi atakapolipa aje na Bank Pay in slip ya malipo ya ada shuleni.

Pay in slip iandikwe jina la mwanafunzi na kidato chake na si jina la mzazi / mlezi aliyeweka fedha benki. Michango yote ikiwa ni pamoja na ada za mitihani ya kitaifa na mock iletwe taslimu shuleni.       

2.0 MAHITAJI MUHIMU;

 

             TAALUMA


·     Oxford Student Dictionary: For learners using English to Study other subjects.

·     Ream mbili (02) A4 za karatasi nyeupe kwa ajili ya photocopy kwa mwaka mzima.

·     Ream moja (01) Ruled papers karatasi za misitari – Kidato cha 3 na 4 tu 

·     Spring files mbili (2) (Moja kwa ajili ya kutunzia mitihani yake na jingine litakabidhiwa kwa mkuu wa shule kwa ajili ya taarifa binafsi za mwanafunzi)

·     Graph Pad Paper moja

·     Kitabu Student’s Companion by Wilfred Best

·     Biblia / Quran (Kadri ya Imani)

·     Four Figure (Mathematical tables)

·     Note book kwa ajili ya Nukuu (Summary) moja kwa kila somo

·     Rula ndefu (Futi moja)

·     Mkebe wa Hisabati (Mathematical Set)

·     Kalamu za wino za kutosha, Penseli na kifutio

·     Vitabu angalau viwili vya masomo yoyote kwa kidato husika – (ni mali ya mwanafunzi)

·     Daftari za kutosha masomo yote zisizopungua 12 (Counter Book Q3 au 4)


MUHIMU: Vifaa vyote hivi vinapatikana kwenye duka la Shule. Tunashauri mwanafunzi anunue vifaa tajwa hapo juu hapahapa shuleni kwa bei nafuu kabisa ambayo si tofauti na ile ya Kasulu mjini. Hii itasaidia kuepuka kununua vifaa tofaiti na mahitaji ya shule. Lakini pia itakupunguzia usumbufu wa kusafiri na mizigo mingi.

 

2.1.  SARE ZA SHULE.

2.1.1.  WAVULANA


-       Suruali mbili za rangi ya zambarau kitambaa kizito (Istimu) Suruali ziwe za heshima na zisiwe za kubana, ziwe na marinda.

-       Mashati mawili meupe mikono mifupi

-       Viatu vyeusi jozi mbili siyo vya visigino virefu

-       Soksi ndefu pea mbili au zaidi rangi nyeusi

-       Mavazi ya michezo; Viatu vya michezo, Bukta na Tshirt ya rangi ya bluu

-       Nguo za kuvaa baada ya masomo (au za kushindia) Suruali 2 nyeusi za kitambaa na siyo mtumba ziwe za heshima

-       Tshirt mbili (2) zinaptikana shuleni (30,000)

-       Truck suit rangi ya Kijani jeshi

-       Sweta rangi ya damu ya mzee.

-       Brash ya Viatu, Kiwi au dawa ya viatu nyeusi

-       Mkanda mweusi wa ngozi

-       Nguo za ndani za kutosha

-       Shuka jozi mbili za rangi ya bluu bahari (Light bluu)

-       Blanketi, mto wa kulalia na foronya

-       Chandarua cha mbu, kiwe kipya

-       Mafuta ya kujipaka

-       Sanduku la chuma (Trunk) na kufuli zake

-       Sabuni za kufulia na kuogea za kutosha

-       Taulo

-       Kandambili / yeboyebo

-       Dawa ya meno na miswaki (3)

-       Tochi ya betri kwa ajili ya dharura wakati umeme unapokuwa umekatika kabla ya kuwasha jenereta

-       Godoro la futi 2½ (Dodoma QFL) au kukodi godoro la shule Tsh. 10,000/- kwa kila muhula.

-       Vyombo vya kulia chakula (Sahani, Bakuli, Kikombe na Kijiko)

-       Dumu la lita 5 la kutunzia maji ya kunywa.


Angalizo: Vifaa vyote viwekewe alama binafsi ya utambulisho

2.1.2. WASICHANA


-     Sketi mbili zenye malinda mapana rangi ya zambarau kitambaa kizito, Sketi ziwe ndefu, zifike chini ya magoti sketi fupi haziruhusiwi.

-     Shati mbili za mikono mifupi

-     Viatu vyeusi jozi mbili siyo vya visigino virefu

-     Mavazi ya michezo: Tshirt rangi ya bluu, Sketi ya Kitambaa cha Sukarisukari rangi nyekundu.

-     Nguo za kuvaa baada ya masomo (au za kushindia) gauni mbili za malinda rangi ya dark bluu zinapatikana shuleni kwa gharama ya Tshs 40,000/= @

-     Brashi ya viatu, Kiwi au dawa ya viatu vyeusi

-     Nguo za ndani za kutosha

-     Taulo za kike (Pedi)

-     Shuka jozi mbili rangi ya bluu bahari (Light blue)

-     Blanketi, Mto wa kulalia na foronya

-     Chandarua cha mbu, Kiwe kipya

-     Mafuta ya kujipaka

-     Sanduku la chuma (Trunk) na kufuli zake

-     Sabuni za kufulia na kuogea za kutosha

-     Tshirt mbili (2) zinapatikana shuleni (30,000/=)

-     Truck suit rangi ya kijani zinauzwa shuleni (30, 000/=)

-     Sweta rangi ya damu ya mzee zinauzwa shuleni (10, 000/=)

-     Taulo na khanga

-     Kandambili / yeboyebo

-     Dawa ya meno na miswaki 3

-     Tochi ya betri kwa ajili ya dharura wakati umeme unapokuwa umekatika kabla ya kuwasha jenereta ya shule

-     Godoro la futi 2½ (Dodoma QFL) au kukodi godoro la shule Tsh. 10,000/- kwa kila muhula.

-     Vyombo vya kulia chakula (Sahani, Bakuli, Kikombe na Kijiko)

-     Dumu la lita 5 la kutunzia maji ya kunywa yaliyochemshwa


 

Angalizo: Vifaa vyote viwekewe alama binafsi ya utambulisho

2.2  VIFAA VYA USAFI


i.       Ndoo na mfagio (Mopa)

ii.      Ndoo ndogo lita 10

iii.    Mfagio (squeezer)

iv.    Mfagio wa nje (chelewa)

v.      Beseni

vi.    Mpini wa jembe la mkono


3.0 VITU VISIVYOTAKIWA SHULENI

i.       Aina yoyote ya manukato (Perfume), Lotion au Vipodozi vyovyote vya kujichubua.

ii.      Simu, Radio, Camera, Mishumaa, Mapambo kama vile hereni, Pete na Mikufu.

iii.    Vitu vyenye ncha kali kama Kisu, Sindano na kadhailika.

4.0 AFYA

Mtoto anatakiwa afanyiwe uchunguzi wa afya kwa daktari wa Hospitali inayotambulika na Serikali. Vielelezo vya afya yake vijazwe kikamilifu kwenye fomu kisha aje na fomu hiyo. Aidha, mtoto mwenye matatizo mengine ya afya aje na vyeti vya udhibitisho na kumbukumbu, fomu ya afya imeambatanishwa na maelekezo haya ya kujiunga na Shule.

Sharti la lazima mtoto awe na Bima ya Afya ama ya jamii iliyoboreshwa (CHF) au ya Taifa (NHF) kwa wale ambao ni wafaidika wanaohudumiwa na Serikali. Shule inatoa huduma ya kwanza tu. Tujenge utamaduni wa kupima afya kila mara kwa watoto wetu hasa kila wanapokuwa likizo.

5.0 UTUNZAJI WA MALI ZA SHULE.

Mwanafunzi atawajibika kutunza vifaa vyote atakavyopewa kutumia shuleni. Yeyote atakayeharibu mzazi / mlezi atawajibika kulipa au kutengeneza uhalibifu utakaokuwa umesababishwa na mwanafunzi husika.

Mwisho shule inakukaribisha sana hapa Magaba Sekondari ili ushiriki kikamilifu katika kukuza vipaji vyako ili vikuwezeshe kuwa Raia mwema na kukua katika Maadili, Uzalendo, Udadisi na Utayari katika kumudu maisha yako na changamoto za kimaisha mbeleni.

 

KARIBU SANA MAGABA SEKONDARI

 

MAWASILIANO: 0767 322707, 0784 555011, 0765 801000

Wako katika elimu

 

-------------------------

Mkuu wa Shule.

SHULE YA SEKONDARI MAGABA

S. L. P. 264, KASULU TANZANIA

TARATIBU ZA SHULE

1.0         SHERIA NA MASHARTI YA SHULE

Kila mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga au kuhamia lazima apime afya yake na kujaza fom iliyoambatanishwa na maelekezo haya na kuirudisha shuleni. Fomu hii ijazwe na Daktari wa serikali mwenye cheo cha Clinical Officer au Medical Officer na kupigwa muhuri.

1.1         TAALUMA:

Lengo la shule ni kuwa kitovu cha taaluma na nidhamu bora na hatimaye kuwa shule bora katika mkoa wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla. Dhima ya shule ni kujenga mazingira bora ya kielimu yanayoheshimu na kujari mahitaji ya watu wote, ili kwamba wanafunzi wetu waweze kupata stadi za kazi zitakazowawezesha kukabiliana na changamoto za kimaisha. Ili kuyafikia haya, kila mwanafunzi hana budi kutimiza na kutekeleza masharti yafuatayo;

a)      Kila mwanafunzi ahudhurie masomo kwa muda wa siku mia moja tisini na nne (194) kwa mwaka, ukiondoa Jumamosi, Jumapili na sikukuu za kitaifa.

b)      Kama kutakuwa na sababu za msingi za mwanafunzi kutofika shuleni wakati wa kufungua shule, ni jukumu la mzazi/mlezi kufika mwenyewe kutoa taarifa kwa mkuu wa shule au kutoa taarifa ya maandishi kwa uongozi wa shule, mapema iwezekanavyo.

c)      Kila mwanafunzi awe ameingia darasani na kukaa katika kiti chake kabla yamwalimu wa somo kuingia na kuanza kufundisha.

d)      Mwalimu aingiapo darasani wanafunzi wote wasimame na kumsalimia.

e)      Wanafunzi wote wawe kimya wakimsikiliza mwalimu wakati akifundishaisipokuwa mwalimu akiuliza swali, akiruhusu mjadala au maigizo darasani.

f)       Kila mwanafunzi ahudhurie vipindi vyote kwa mujibu wa ratiba ya siku.

g)       Kila mwanafunzi afanye mazoezi na mitihani yote anayopewa na walimu wamasomo mbalimbali katika muda aliopewa.

h)     Kila mwanafunzi afikie wastani wa asilimia arobaini na tano (45%), kilamwisho wa mwaka wa masomo. Mwanafunzi atakayeshindwa kufikia kiwangohicho, atalazimika kukariri darasa

i)       Mwanafunzi yeyote ambaye atakwepa kufanya mitihani au zoezi la somololote la kidato husika bila ruhusa iliyoidhinishwa na Mkuu wa shule, hatapewaalama yoyote na badala yake ataandikiwa sifuri katika somo hilo na alama hiyo itajumlishwa katika kutafutawastani wake wa mwisho wa muhula au mwaka.

j)       Mwanafunzi haruhusiwi kuibia mitihani kutoka kwa mwanafunzi mwenzake au kwenda chumba cha mtihani na majibu yaliyoandikwa kwenye karatasi, nguo rula n.k. au kuongea na mwanafunzi mwenzake kwenye chumba chamitihani wakati mtihani ukifanyika. Atakayebainika kukiuka sheria hii ya shule, atapata adhabu ya kusimamishwa masomo na hatimaye kufukuzwa shule.

k)      Kila mwanafunzi awe na daftari la mazoezi/majaribio kwa kila somo.

 

2.0 NIDHAMU

Shule ya sekondari Magaba inaamini kuwa Nidhamu Bora ni Ufunguo wa Taaluma Bora. Kwa hiyo, inahimiza sana juu ya umuhimu wa wanafunzi kuwa na nidhamu bora. Kama sehemu ya nidhamu bora, kila mwanafunzi anapaswa:

a)    Awe amefika Smart area kabla ya saa moja na dakika ishirini asubuhi akiwa katika sare rasmi ya shule iliyo safi.

b)      Awahi kuhudhuria Mkutano wa Asubuhi na mchana (School Assembly) au mikutano ya asubuhi ya darasa kwa siku na wakati husika.

c)      Awepo mahali husika kwa mujibu wa ratiba ya siku hiyo.

 

3.0 AFYA NA USAFI

Afya na Usafi ni sehemu muhimu ya Taaluma na Nidhamu bora. Kwa hiyo, ni lazima: -

a)    Kila mwanafunzi aonekane nadhifu wakati wote.

b)    Mwanafunzi ashiriki katika kusafisha na kutunza mazingira ya shule ikiwa ni pamoja na kufagia /kudeki vyumba vya madarasa, kuondoa buibui, kufuta vumbi kwenye vioo, milango, madirisha n.k. kila atakapotakiwa kufanya hivyo.

c)    Kila mwanafunzi atunze vifaa vya kufanyia Usafi, atakavyokabidhiwa. Upotevu au uharibifu wa vyombo hivyo utagharimiwa na mwanafunzi ambaye atakuwa amehusika na uharibifu au upotevu wa vifaa hivyo.

 

4.0 TABIA NA MWENENDO

Kila mwanafunzi anatakiwa afanye yafuatayo:

a)      Mwanafunzi anatakiwa kuwasalimu wafanyakazi wote wa shule atakaokutana nao ndani na nje ya shule.

b)      Wanafunzi wote wanapaswa kuheshimu, kusimama kwa ukakamavu, kuwa kimya wakati wimbo wa taifa unaimbwa na wakati bendera ya taifa inapopandishwa au kuteremshwa.

c)      Mwanafunzi anatakiwa kupokea /kutii amri zote halali zitolewazo na utawala wa shule bila ubishi.

d)      Mwanafunzi HARUHUSIWI kutumia lugha ya matusi.

e)      Ni marufuku kupiga kelele au kuleta usumbufu wa aina yoyote bwenini, darasani au nje ya darasa.

f)       Ni marufuku mwanafunzi kutoka nje ya shule wakati wa masomo bila ya ruhusa toka kwa Mkuu wa shule au waandamizi wake.

g)      Kila mwanafunzi atawajibika kutunza mali yake binafsi pamoja na ile ya shule na kutoa taarifa kwa utawala wa shule endapo mali hizo zitaharibiwa/kuibiwa.

h)     Mwanafunzi haruhusiwi kuja shuleni na vitu vya thamani kubwa vinavyoweza kuathiri tabia na mwenendo wake kitaaluma na kinidhamu; kama vile simu za mkononi, redio, kamera, sistimu ya video, kompyuta ndogo (laptops) au fedha nyingi kuliko mahitaji yake.

i)       Ni marufuku mwanafunzi kuiba mali ya mwenzake au ya shule.

 

5.0 SHERIA ZA BWENI


a)      Zungumza lugha ya Kiingereza wakati wote

b)      Kupiga kelele hairuhusiwi

c)      Dumisha usafi bwenini

d)      Tandika kitanda chako na kuhakikisha ni kisafi daima

e)      Hakikisha mabomba ya maji yamefungwa na hayatoi maji ovyo. Pia hakikisha taa zote zimezimwa pale ambapo hazihitajiki kwa wakati huo.

f)       Weka vifaa vyako kwenye begi na sanduku lako

g)      Usitundike nguo zako ukutani, kitandani wala dirishani

h)     Weka viatu vyako kwa mpangilio chini ya kitanda chako

i)       Lala kwenye kitanda ulichopewa tu na siyo vinginevyo

j)       Redio haziruhusiwi bwenini

k)      Simu za mkononi (mobile phones) haziruhusiwi shuleni/bwenini

l)       Vaa nguo za heshima uwapo bwenini na hasa nguo zilizoruhusiwa

m)    Mapambo na vitu vingine kama mikufu, shanga nk haviruhusiwi

n)     Hairuhusiwi kuandika maandishi yoyote ukutani.

o)      Hairuhusiwi kununua vyakula vya aina yoyote kutoka nje ya maeneo yanayolizunguka bweni

p)      Lugha ya matusi hairuhusiwi ndani na nje ya bweni

q)      Hairuhusiwi kunywa kileo cha aina yoyote, kuvuta sigara au madawa ya kulevya.

r)      Hairuhusiwi kuvunja au kuharibu kitu chochotekilicho mali ya bweni (shule)

s)       Hairuhusiwi kulala bwenini kwa kuumwa bila kibali cha matron au patron wa shule.

t)       Hairuhusiwi kulala wanafunzi zaidi ya mmoja kwenye kitanda kimoja

u)     Hairuhusiwi kulala kwenye kitanda kisicho chako.

v)      Hakuna mwanafuzni atakayeruhusiwa kwenda nje ya eneo la shule bila ruhusa ya Mkuu wa shule.

w)    Wakati wa kusafiri, kila mwanafunzi atavaa sare za shule.

x)      Vifaa vyote atakavyokuja navyo mwanafunzi vitakaguliwa wakati wa udahili.

y)      Chakula toka nje hakiruhusiwi shuleni. Wanafunzi wote watakula chakula kitakachotolewa shuleni.


 

MAKOSA YAFUATAYO NI YA KUMFUKUZA MWANAFUNZI SHULENI.


i.          Kupiga / Kupigana

ii.         Wizi wa kila aina, iwe wa kutumia nguvu au udanganyifu.

iii.       Uasherati na kila aina ya tabia inayohusiana na mahusiano ya kimapenzi.

iv.       Ulevi wa aina yoyote na uvutaji wa sigara / bangi / kuberi na kadhalika.

v.         Makosa ya jinai

vi.       Kuharibu kwa makusudi mali za umma / shule / mwanafunzi

vii.      Kudharau alama za Taifa (Bendera na Wimbo wa Taifa)

viii.    Kusababisha, Kubeba au kutoa mimba / kuwa mjamzito au kusababisha ujauzito ndani au nje ya shule.

ix.       Kuoa au kuolewa / kuwekwa kimada /ushoga

x.         Utoro wa mfululizo

xi.       Wizi wa mitihani

xii.      Aina yoyote ya uonevu kwa mwanafunzi mwenzako

xiii.    Kutumia lugha chafu kwa Wafanyakazi /wanafunzi wenzako

xiv.    Kutoka nje ya shule au kuingia shuleni bila taarifa yoyote

xv.      Kutoroka shuleni mchana na usiku / kuruka ukuta au uzio kutoka nje ys shule

xvi.    Kuingia katika majumba ya starehe

xvii.   Kuwa na Simu/ Redio uwapo shuleni

xviii. Kugoma na kuvuruga amani na usalama wa watu shuleni


 

ANGALIZO

·        Sheria hizi zimetungwa kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa mujibu wa Wizara ya Elimu, na Mafunzo ya Ufundi.

·        Pia, sheria zote zinalenga kumjenga mwanafunzi kiakili na kimaadili ili hatimaye aweze kulitumikia Taifa kwa uadilifu na kuwa raia mwema.

·         Sheria nyingi za bweni hutungwa kufuatana na sheria za nchi. Aidha baadhi ya sheria hutungwa kwa kuzingatia mazingira ya shule na kanuni za wizara ya Elimu zinazohusu uendeshaji wa Shule za Sekondari. Kila mwanafunzi anapaswa kuzisoma na kuzielewa sheria hizo kwa nia ya kuzifuata.

·        Uvunjaji wa sheria za shule unaweza kusababisha mwanafunzi kupewa adhabu au kufukuzwa shule

·        Utii wa kengele ni jambo muhimu sana kila mwanafunzi anahimizwa azingatie.

·        Sheria hizi zina lengo la kuleta amani na utulivu shuleni hivyo kila mwanafunzi ni lazima azifuate.

 

Wako katika elimu

 

-------------------------

Mkuu wa Shule.

 

 

 

 

(Sheria za shule hizi ni nakala ya mwanafunzi na anapaswa abaki nazo na azisome mara kwa mara ili azielewe na kuziishi)

F. 01

MAGABA SECONDARY SCHOOL

MEDICAL EXAMINATION FORM    

(To be filed by an Authorized Government Medical Officer and returned to school)

TO THE MEDICAL OFFICER

__________________________________________________________________________________

__________________________________________________________________________________

__________________________________________________________________________________

RE: Master / Miss ___________________________________________________________________

Please examine the above student as to her/his physical fitness for a full time schooling course. The examination should include categories a - n. Each category of which will render the applicant ineligible of defect.

MEDICAL CERTIFICATE

_____________________________________________ have examined the above subject and consider that he / she is physically fit / unfit for a full time schooling course.

(a)    Eye sight ________________________________________________________________________________

(b)    Hearing _________________________________________________________________________________

(c)    Limbs __________________________________________________________________________________

(d)    Speech _________________________________________________________________________________

(e)    Venereal Disease __________________________________________________________________________

(f)     Leprosy _________________________________________________________________________________

(g)    Epilepsy ________________________________________________________________________________

(h)    Asthma _________________________________________________________________________________

(i)     Heart Problem ____________________________________________________________________________

(j)     Kidney __________________________________________________________________________________

(k)    Peptic Ulcers _____________________________________________________________________________

(l)     Sickle cell anemia _________________________________________________________________________

(m)     TB ____________________________________________________________________________________

(n)    Chronic Malaria __________________________________________________________________________

(o)    Neurosis ________________________________________________________________________________

(p)    Other serious disease ______________________________________________________________________

 

Date _________________________________                                          Signature _____________________

Official stamp of the Hospital                                                                      Designation ___________________

 

(Fomu hii iikabidhiwe shuleni kwa mkuu wa shule kwa ajili ya matumizi ya ofisi)

F. 02

SHULE YA SEKONDARI MAGABA

S. L. P 264, KASULU TANZANIA

FOMU YA KUORODHESHA NDUGU WATAKAOMTEMBELEA MTOTO SHULENI

 

Ndugu mzazi / mlezi _________________________________________________________

Shule ya Sekondari Magaba inakutaarifu kuwa mwanao atakapojiunga na shule hii atapewa muda wa kuonana na kuongea na ndugu zake kwa muda utakaopangwa. Itapangwa tarehe maalumu toka kwa 0fisi ya Mkuu wa shule. Kwa hiyo, shule hii inapenda kuwafahamu ndugu watakaomtembelea mwanao akiwa shuleni. Uongozi wa shule unakushauri uwachague kwa makini na uwaorodheshe katika fomu hii. Fomu hii lazima irudishwe shuleni kwa ajili ya utekelezaji wa maadili ya vijana.

 

No.

JINA

UHUSIANO

1

 

 

2

 

 

3

 

 

4

 

 

 

Mimi ____________________________ Mzazi / Mlezi wa ______________________________

Nimeidhinisha watu wenye majina yaliyoandikwa hapo juu kumtembelea mwanangu kulingana na taratibu zilizowekwa na shule ya sekondari Magaba. Mtu yeyote mwingine ambaye hayuko kwenye orodha hii, atakuja kumtembelea mwanangu baada ya kupewa ruhusa na mimi mwenyewe na kuujulisha uongozi wa shule. Endapo atatokea mtu yeyote kuja kumuona mwanangu bila ruhusa yangu nijulisheni mara moja.

Namba yangu ya simu ni ______________________________

 

 

 

 

 

 

(Fomu hii iikabidhiwe shuleni kwa mkuu wa shule kwa ajili ya matumizi ya ofisi)

 

PICHA YA MWANAFUNZI

F. 03

SHULE YA SEKONDARI MAGABA

S. L. P 264, KASULU TANZANIA

 

MAELEKEZO.

 

Jaza fomu hii kwa usahihi tumia herufi kubwa.

Fomu hii pamoja na risiti ya malipo virudishwe shuleni mwanafunzi anapokuja kuripoti.

 

1.     Jina la mwanafunz:i _____________________________________________(majina matatu)

2.     Tarehe ya kuzaliwa: __________________        Wilaya ___________    Mkoa: _______________

3.     Sehemu anayoishi sasa ________________Wilaya:______________  Mkoa _________________

4.     Dini _________________ Dhehebu ______________________________

5.     Mwaka wa kumaliza darasa la saba ____________________

6.     Jina la shule ya msingi __________________________________________

7.     Jina la shule ya sekondari aliyokuwa akisoma ____________________________________________

8.     Jina kamili la mzazi / mlezi __________________________________________

9.     Kazi ya mzazi / mlezi ________________________________________

10.  Anuani ya mzazi / mlezi __________________________________

                                         _________________________________

11.  Namba ya simu ya mzazi / mlezi( kwa ajili ya mawasiliano)  _____________________________

12.  Barua pepe (E-mail) _______________________________________

 

 

 

TAMKO LA MWANAFUNZI:

 

Mimi _____________________________________ nimesoma kwa makini sheria, taratibu na maelekezo ya shule na kuelewa. Nakubaliana na vyote na naahidi kuvifuata vyote kwa kadiri ya uwezo wangu. Nakubali kwamba endapo nitajiingiza katika tatizo la uvunjaji wa sheria au utaratibu wowote, hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yangu.

Jina__________________________________ Saini: ____________________ Tarehe: ______________

TAMKO LA MZAZI:

a)     Mtoto wangu akipata nafasi kujiunga na shule hii itabidi afuate taratibu, sheria na kanuni za shule ya sekondari Magaba.

b)     Ninakubali kumlipia karo (ada) ya shule na gharama zingine anazostahili ili kumwezesha kusoma bila tatizo, asiache masomo yake kwa ajili ya ukosefu wa mahitaji mbalimbali.

c)     Nitashirikiana na uongozi wa shule katika kumsaidia mwanangu kitaaluma na nidhamu.

Jina la mzazi / mlezi: _______________________   Saini: ___________    Tarehe: _____________

Namba ya simu: ____________________________________

 

 

(Fomu hii iikabidhiwe shuleni kwa mkuu wa shule kwa ajili ya matumizi ya ofisi)




0 comments:

Post a Comment