Tuesday, June 11, 2024

Walimu Magaba sec wanolewa ki-TEHAMA

 


Timu ya walimu wa shule ya sekondari Magaba wamepewa mafunzo maalumu ya matumizi ya teknolojianys Habari na Mawasiliano ili kuboresha taaluma shuleni

Mafunzo hayo yamefanyika leo katika makao makuu ya shule hiyo iliyopo Nyakitonto wilayani kasulu ambalo walimu watano na mwendesha ofisi wameshiriki

Akitoa mafunzo hayo mkufunzi kutoka buha media Bw. Prosper Kwigize ametambulisha tovuti mpya ya shule na kuwaelekeza walimu namna ya kuitumia kuitangaza shule na kusisimua taaluma kwa wazazi, wanafunzi na jamii

Walimu hao wamefundishwa namna ya kuandika habari zitakazovutia wazazi kupeleka watoto katika shule hiyo sambamba na kuamsha Ari ya masomo kwa wanafunzi

Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Mkurugenzi wa shule ya Magaba Sekondari Bw. Leonard Magaba kama sehemu ya mkakati wa maboresho ya mfumo wa ufundishaji na ushaeidhi wa jamii kujali Elimu.

0 comments:

Post a Comment