Latest Posts
Friday, October 18, 2024
Wednesday, June 12, 2024
Walimu na watumishi kutoka idara ya utawala ya Magaba Secondary iliyopo Kasulu wamefanya ziara ya mafunzo katika kituo cha habari cha Buha, wamefurahishwa na mfumo wa TEHAMA na uandishi wa habari za elimu.
https://web.facebook.com/share/p/ke1g5dhFD5voBBr3/Tuesday, June 11, 2024
Timu ya walimu wa shule ya sekondari Magaba wamepewa mafunzo maalumu ya matumizi ya teknolojianys Habari na Mawasiliano ili kuboresha taaluma shuleni
Mafunzo hayo yamefanyika leo katika makao makuu ya shule hiyo iliyopo Nyakitonto wilayani kasulu ambalo walimu watano na mwendesha ofisi wameshiriki
Akitoa mafunzo hayo mkufunzi kutoka buha media Bw. Prosper Kwigize ametambulisha tovuti mpya ya shule na kuwaelekeza walimu namna ya kuitumia kuitangaza shule na kusisimua taaluma kwa wazazi, wanafunzi na jamii
Walimu hao wamefundishwa namna ya kuandika habari zitakazovutia wazazi kupeleka watoto katika shule hiyo sambamba na kuamsha Ari ya masomo kwa wanafunzi
Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Mkurugenzi wa shule ya Magaba Sekondari Bw. Leonard Magaba kama sehemu ya mkakati wa maboresho ya mfumo wa ufundishaji na ushaeidhi wa jamii kujali Elimu.